Changisha SW EN

Kuchangisha fedha za matibabu

Bili ya hospitali, upasuaji, dawa au matibabu nje ya mkoa — anzisha kampeni ya matibabu na uwaruhusu ndugu, marafiki na hata watu wasiokujua kuchangia kwa mobile money.

Nyaraka zinazohitajika

Pamoja na nyaraka hizi, mmiliki wa kampeni anathibitisha utambulisho wake kwa NIDA, picha ya kitambulisho na selfie. Ukichangisha kwa ajili ya mgonjwa mwingine, utahitaji pia ridhaa yake.

Jinsi ya kuandika kampeni ya matibabu inayoaminika

Fedha zinaweza kwenda moja kwa moja hospitali?

Ndiyo. Akaunti ya kupokea fedha inaweza kuwa ya mgonjwa au ya hospitali husika, na inathibitishwa wakati wa kukagua kampeni. Benki inapokea kiasi chote kwa mara moja; mobile money inapokea hadi TZS 5,000,000 kwa siku.

Kampeni zinazoendelea

WEZESHA ADA YA SHULE

Ndugu jamaa, marafiki na wadau, Natumaini mko salama. Naomba msaada wenu wa kifedha ili kufanikisha malipo…

TZS 9,500 / TZS 1,000,000
Changia

Maswali ya mara kwa mara

Kampeni ya matibabu inaidhinishwa kwa muda gani?

Mara tu nyaraka zote zikiwa zimepakiwa na utambulisho wako umethibitishwa, timu yetu inakagua — mara nyingi tunapiga simu hospitali kuthibitisha. Kamilisha nyaraka mapema ili kampeni ianze haraka.

Je, mchangiaji anahitaji akaunti?

Hapana. Anachagua kiasi, anaweka namba ya simu na kuthibitisha kwa PIN ya M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa.

Ada ni kiasi gani?

Kuanzisha kampeni ni bure. Mchangiaji analipa ada ya huduma juu ya mchango (5% + takriban 2.57% ya mtandao), hivyo mgonjwa anapokea mchango wote.

Uko tayari kuanza?

Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Maswali? Tupigie 0678515121

Anzisha kampeni

Miongozo mingine