Kuchangisha ada ya shule au chuo
Ada, sare, vitabu, hosteli au ada ya chuo — kampeni ya elimu inakusaidia kukusanya michango kutoka kwa familia, marafiki, wahitimu na wadau wa elimu.
Nyaraka zinazohitajika
- Barua ya kujiunga / fee structure ya shule au Makadirio ya gharama / invoice
- Picha ya hali halisi (mlengwa / tukio)
- Barua ya Serikali ya Mtaa / Mtendaji wa Kata
Vidokezo vya kampeni ya elimu
- Taja shule au chuo, kidato au mwaka wa masomo, na kipindi ambacho ada inahitajika.
- Weka lengo linalolingana na fee structure au invoice ya shule.
- Eleza ndoto za mwanafunzi na matokeo yake — wachangiaji wanapenda kuona tofauti watakayoleta.
- Shule au taasisi inaweza kuchangisha kwa ajili ya wanafunzi wengi, mf. "ada za wanafunzi 40 muhula huu".
Fedha zinaweza kulipwa shuleni moja kwa moja?
Ndiyo. Akaunti ya kupokea fedha inaweza kuwa ya shule au chuo husika, na inathibitishwa pamoja na kampeni. Hii inawapa wachangiaji uhakika kwamba fedha zitatumika kwa ada.
Kampeni zinazoendelea
WEZESHA ADA YA SHULE
Ndugu jamaa, marafiki na wadau, Natumaini mko salama. Naomba msaada wenu wa kifedha ili kufanikisha malipo…
Changia
Maswali ya mara kwa mara
Nani anaweza kuanzisha kampeni ya ada?
Mwanafunzi mwenyewe (mtu mzima), mzazi, mlezi au mtu mwingine kwa ridhaa ya mlengwa — pamoja na shule na taasisi zilizosajiliwa.
Lengo la chini ni kiasi gani?
Lengo la kampeni ni angalau TZS 100,000.
Wachangiaji wanalipaje?
Kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa — bila akaunti wala app.
Uko tayari kuanza?
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Maswali? Tupigie 0678515121