Michango ya ujenzi wa kanisa au msikiti
Taasisi za dini zilizosajiliwa zinapata ukurasa wao uliothibitishwa kwenye CHANGISHA: mfuko wa jumla wa michango ya kila siku, na kampeni maalum kwa kila mradi — ujenzi, ukarabati, vyombo au huduma za jamii.
Mnachopata
- Ukurasa wa kudumu (changisha.co.tz/o/jina-lenu) wenye alama ✓ ya uthibitisho.
- Mfuko wa jumla usio na tarehe ya mwisho, kwa michango ya kila siku.
- Kampeni nyingi kadiri mnavyotaka — kila mradi na lengo, picha na maendeleo yake.
- Bango lenye QR code la kuweka kanisani au msikitini: waumini wanascan na kuchangia papo hapo.
- Timu: mweka hazina na kamati wanaweza kupewa nafasi tofauti (kukagua, kuangalia, au kusimamia).
Mahitaji ya usajili
- Cheti cha usajili wa taasisi na cheti cha TIN.
- Barua ya viongozi (bodi au kamati) inayomteua msimamizi wa akaunti.
- Utambulisho wa msimamizi: NIDA, picha ya kitambulisho na selfie.
- Akaunti ya kupokea fedha kwa jina la taasisi — inathibitishwa pamoja na taasisi.
- Kwa kila kampeni ya mradi: andiko la mradi au bajeti na picha halisi.
Kampeni zinazoendelea
Jenga CHANGISHA APP — tusaidie kuendesha jukwaa la kuchangia la Kitanzania
CHANGISHA APP ni jukwaa la Kitanzania linalomwezesha mtu yeyote mwenye uhitaji halisi — matibabu, ada za shul…
WEZESHA ADA YA SHULE
Ndugu jamaa, marafiki na wadau, Natumaini mko salama. Naomba msaada wenu wa kifedha ili kufanikisha malipo…
Maswali ya mara kwa mara
Waumini wanachangiaje?
Wanascan QR code au kufungua link, wanachagua kiasi na kuthibitisha kwa PIN ya M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa. Hakuna app wala akaunti.
Fedha zinaingia kwenye akaunti gani?
Kwenye akaunti ya taasisi tu, iliyothibitishwa wakati wa usajili — si kwenye akaunti ya mtu binafsi.
Tunaweza kuona orodha ya waliochangia?
Ndiyo. Mnaona kila mchango na mnaweza kupakua ripoti ya Excel au PDF kwa ajili ya kamati na waumini.
Uko tayari kuanza?
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Maswali? Tupigie 0678515121