CHANGISHA APP
Kuhusu sisi

Changia, badilisha maisha — kwa uwazi.

CHANGISHA APP ni jukwaa la Kitanzania linalomwezesha mtu yeyote au taasisi kuchangisha fedha mtandaoni kwa matibabu, ada za shule, misiba, dharura na miradi ya jamii. Wachangiaji hulipa kwa mobile money, na kila shilingi inaonekana.

Inavyofanya kazi

Vipengele vyote →
1

Anzisha kampeni

Jisajili, eleza changamoto yako, weka lengo la fedha na picha halisi. Pakia nyaraka za ushahidi na barua ya Serikali ya Mtaa.

2

Tunakagua

Timu yetu inathibitisha NIDA yako, nyaraka na akaunti ya malipo — mara nyingi kwa kupiga simu hospitali, shule au kiongozi wa mtaa. Ikikubaliwa inapata alama ✔.

3

Share na pokea michango

Share link kwenye WhatsApp na mitandao ya kijamii. Wachangiaji hulipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa — progress inaonekana papo hapo.

Ada zetu — wazi kabisa

Ada ya huduma
Ada ya jukwaa 5% + gharama ya mtandao wa malipo (~2.57%)
Inalipwa na mchangiaji juu ya mchango
Bahshishi (tip)
Hiari kabisa — 0%, 5%, 10% au 15%
Inatusaidia kuendesha jukwaa; unaweza kuchagua "Hapana"
Ada ya kutoa fedha
Kwa kila ombi la malipo la mwenye kampeni
TZS 1,500 · kiwango cha chini cha kutoa TZS 10,000
Kufungua akaunti na kampeniBure

Kwa sababu ada inalipwa na mchangiaji, kampeni inapokea mchango wote uliouchagua.

Kwa nini uamini kampeni za CHANGISHA APP

Utambulisho wa NIDA

Kila mwenye kampeni anathibitisha simu kwa SMS, kisha NIDA, picha ya kitambulisho na selfie akiwa amekishika.

Nyaraka na picha halisi

Barua ya hospitali au shule, makadirio ya gharama, picha ya hali halisi na barua ya Serikali ya Mtaa — tunazikagua moja moja.

NGO zilizothibitishwa

Taasisi huwasilisha cheti cha usajili, TIN na barua ya viongozi. Zikithibitishwa hupata alama ✔ na ukurasa wao wenyewe. Mwongozo kwa taasisi →

Malipo kwa awamu

Fedha hutolewa kwa akaunti iliyokaguliwa tu, kwa awamu hadi TZS 1,000,000. Awamu inayofuata inahitaji risiti za matumizi, na kiasi kilichotolewa kinaonekana hadharani.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, ninahitaji akaunti ili kuchangia?

Hapana. Weka kiasi, jina na namba ya simu, kisha thibitisha kwa PIN yako ya mobile money. Utapokea ujumbe wa asante wenye kumbukumbu ya muamala.

Mwenye kampeni anapokea fedha lini?

Baada ya kampeni kuthibitishwa, anaweza kuomba malipo wakati wowote (kiwango cha chini TZS 10,000, ada TZS 1,500 kwa ombi). Kampeni inaendelea kupokea michango wakati huo.

Je, naweza kuchangia bila jina langu kuonekana?

Ndiyo. Chagua "Ficha jina langu" — kwenye ukurasa wa kampeni utaonekana kama "Mfadhili".

Nikiona kampeni ya udanganyifu nifanye nini?

Bonyeza "Ripoti kampeni hii" chini ya fomu ya kuchangia. Tunasimamisha malipo na kuchunguza kila ripoti.

Ada ya huduma inatumika kwa nini?

Kulipia mitandao ya malipo, SMS na WhatsApp, ukaguzi wa kampeni na uendeshaji wa jukwaa.

Una swali? Tuko hapa.

Simu: 0678515121 · Barua: info@changisha.co.tz

Anzisha kampeni