Pokea michango mtandaoni — kwa uwazi unaojenga imani.
NGO, CBO, taasisi za dini, foundation na shule zinapata ukurasa wao wenyewe wenye alama ✔, mfuko wa kuchangia usio na tarehe ya mwisho, na kampeni maalum kwa kila mradi. Wafadhili wanalipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa.
Mnachopata
Ukurasa wa taasisi
Link yenu ya kudumu (changisha.co.tz/o/jina-lenu) yenye historia yenu, alama ✔, takwimu za michango, kampeni zenu na mawasiliano.
Mfuko wa jumla
Kitufe cha "Changia" kwenye ukurasa wenu — kinapokea michango wakati wowote, bila tarehe ya mwisho, kwa ajili ya kazi za kila siku za taasisi.
Kampeni za miradi
Anzisheni kampeni nyingi kadiri mnavyotaka — kila moja na lengo, picha na progress yake — zote chini ya jina la taasisi.
Hatua kwa hatua
- Fungua akaunti
Jisajili na uchague "Taasisi / NGO". Msimamizi wa akaunti (mtu atakayesimamia kampeni) anatumia jina lake na namba yake ya simu, kisha anathibitisha simu kwa SMS.
- Jaza taarifa za taasisi
Jina kamili kama lilivyo kwenye cheti, namba ya usajili, mamlaka iliyosajili, TIN, mkoa, simu, maelezo ya kazi zenu, logo na picha ya bango.
- Weka akaunti ya kupokea fedha
Mobile money au benki — lazima iwe kwa jina la taasisi. Fedha za taasisi hazilipwi kwenye akaunti ya mtu binafsi.
- Pakia nyaraka
- Cheti cha usajili wa taasisi
- Cheti cha TIN cha taasisi
- Barua ya viongozi (bodi) kuidhinisha msimamizi wa akaunti
- Katiba ya taasisi (hiari)
- Utambulisho wa msimamizi: NIDA, picha ya kitambulisho na selfie
- Wasilisha kwa ukaguzi
Timu yetu inakagua nyaraka, inahakiki usajili kwenye daftari la Msajili na kupiga simu ofisi yenu. Mtajulishwa kwa SMS taasisi ikithibitishwa — au tukihitaji marekebisho.
- Anzeni kupokea michango
Baada ya kuthibitishwa: ukurasa wenu wa umma unafunguka na mfuko wa jumla unaanza kupokea michango. Share link kwenye WhatsApp, Facebook na kwa wanachama wenu.
Kampeni maalum za miradi
Kwa mradi wenye lengo maalum (mf. kujenga darasa, kununua vifaa, ada za wanafunzi 40), anzisheni kampeni na mchague "taasisi" kama mmiliki. Kampeni ya taasisi inahitaji:
- Picha halisi ya mradi au walengwa
- Andiko la mradi au bajeti inayoonyesha fedha zitatumikaje
Barua ya Serikali ya Mtaa haihitajiki kwa kampeni za taasisi iliyothibitishwa — usajili wenu unatosha. Kila kampeni bado inakaguliwa kabla ya kuanza kupokea michango.
Kupokea fedha
Kuomba malipo
Ombeni malipo wakati wowote kutoka kwenye mfuko wa jumla au kampeni. Ada ya kutoa ni TZS 1,500 kwa kila ombi; kiwango cha chini ni TZS 10,000.
Uwajibikaji
Kiasi kikubwa hulipwa kwa awamu hadi TZS 1,000,000; awamu inayofuata baada ya kupakia risiti za matumizi. Kiasi kilichotolewa kinaonekana hadharani kwenye ukurasa wenu.
Ada
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Mfadhili analipa ada ya huduma juu ya mchango wake, hivyo taasisi inapokea mchango wote. Ona ada zetu →
Taarifa
Mnapata ujumbe kwa kila mchango unaoingia; wafadhili wanapata risiti ya asante yenye kumbukumbu ya muamala.
Maswali ya mara kwa mara
Ni taasisi gani zinaweza kujisajili?
NGO, CBO, taasisi za dini (makanisa, misikiti), foundation/mifuko, shule na vyuo — yoyote iliyosajiliwa rasmi Tanzania na yenye TIN.
Uthibitisho unachukua muda gani?
Inategemea ukamilifu wa nyaraka zenu. Nyaraka zikiwa wazi na zinazolingana, ukaguzi huwa wa haraka; tukihitaji marekebisho tutawaeleza kwa SMS.
Tunaweza kubadilisha akaunti ya kupokea fedha?
Ndiyo, kupitia ukurasa wa taasisi. Kwa usalama, kubadilisha akaunti ya malipo, jina au usajili hurudisha taasisi kwenye ukaguzi kabla ya malipo mapya kutoka.
Watu wengi wa taasisi wanaweza kusimamia akaunti?
Kwa sasa akaunti moja inasimamiwa na msimamizi mmoja aliyeidhinishwa na barua ya viongozi. Mkibadilisha msimamizi, wasiliana nasi.
Mfadhili anahitaji akaunti?
Hapana. Anaweka kiasi, jina na namba ya simu, kisha anathibitisha kwa PIN yake ya mobile money.
Tayari kuanza?
Maswali? Simu: 0678515121 · Barua: info@changisha.co.tz