Jamii
Imethibitishwa
Jenga CHANGISHA APP — tusaidie kuendesha jukwaa la kuchangia la Kitanzania
1 wafadhili · 0% ya lengo · inaisha 30 Apr 2027
Habari za kampeni
CHANGISHA APP ni jukwaa la Kitanzania linalomwezesha mtu yeyote mwenye uhitaji halisi — matibabu, ada za shule, misiba, dharura au miradi ya jamii — kuchangisha fedha mtandaoni kwa uwazi na usalama. Kila kampeni hukaguliwa (NIDA, nyaraka, barua ya Serikali ya Mtaa), wachangiaji hulipa kwa mobile money, na kila shilingi inaonekana.
Leo tunakuomba utuchangie sisi wenyewe, ili tuendeshe na kukuza jukwaa hili kwa miezi sita ya mwanzo.
Bajeti ya miezi 6 ya kuendesha CHANGISHA — TZS 22,500,000
(gharama kwa mwezi × miezi 6)
• Mishahara ya timu: msanidi wa mfumo (TZS 1,200,000) + afisa wa uthibitisho na huduma kwa wateja (TZS 700,000) — TZS 1,900,000 × 6 = TZS 11,400,000
• Ofisi, intaneti na huduma — TZS 550,000 × 6 = TZS 3,300,000
• Uhamasishaji na elimu kwa jamii (mitandao, redio, vipeperushi) — TZS 400,000 × 6 = TZS 2,400,000
• SMS na WhatsApp (OTP, risiti kwa wachangiaji, taarifa kwa wenye kampeni) — TZS 300,000 × 6 = TZS 1,800,000
• Ukaguzi wa kampeni (usafiri, simu kwa hospitali, shule na viongozi wa mtaa) — TZS 150,000 × 6 = TZS 900,000
• Server, backup na usalama wa mfumo — TZS 100,000 × 6 = TZS 600,000
• Domain na email (changisha.co.tz) — TZS 25,000 × 6 = TZS 150,000
• Usajili, leseni na ushauri wa kisheria (mara moja) — TZS 800,000
• Akiba ya dharura (~5%) — TZS 1,150,000
Jumla: TZS 22,500,000 — wastani wa TZS 3,750,000 kwa mwezi.
Baada ya miezi sita: lengo letu ni jukwaa lijiendeshe kwa ada ya huduma (5% ya michango) na bahshishi za hiari. Kwa mfano, michango ya takriban TZS 75,000,000 kwa mwezi kupitia CHANGISHA ingelipia gharama hizi zote bila kuomba msaada tena.
Uwazi: tutatoa ripoti ya matumizi kila mwezi hapa kwenye ukurasa huu, na kiasi kilichotolewa kinaonekana hadharani kama kampeni nyingine zote.
Kila mchango — hata TZS 1,000 — unatusaidia kuwafikia watu wengi zaidi wanaohitaji msaada. Asante kwa kujenga CHANGISHA pamoja nasi!
—
CHANGISHA APP is a Tanzanian platform that helps anyone with a genuine need raise money online, transparently and safely. We are raising TZS 22,500,000 to run the platform for its first six months (about TZS 3,750,000 a month): the team that builds it and verifies every campaign, office and internet, SMS & WhatsApp notifications, servers, outreach, legal registration and a small reserve. After that, the 5% service fee on donations is meant to cover these costs. Monthly spending reports will be posted here. Thank you!
Wafadhili wa hivi karibuni
MRISHO MARO
Mbarikiwe Sana
2 saa zilizopita
TZS 2,000