CHANGISHA APP
Vipengele

Kila kitu unachohitaji kuchangisha — mahali pamoja.

Kutoka kuanzisha kampeni hadi kupokea fedha: kuchangia kwa mobile money, uthibitisho unaojenga imani, kurasa za taasisi, picha za kushare, taarifa za WhatsApp na ripoti wazi.

Kwa wachangiaji

Kuchangia ni rahisi, salama na wazi — hakuna akaunti inayohitajika.

Lipa kwa mobile money

M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa. Unapokea ujumbe wa PIN kwenye simu yako na unabaki kwenye ukurasa wetu wenye nembo yetu.

Ada wazi kabla ya kulipa

Unaona mchango, ada ya huduma na jumla kabla ya kulipa. Kampeni inapokea mchango wako wote.

Changia bila jina

Chagua "Ficha jina langu" — utaonekana kama "Mfadhili" hadharani. Unaweza pia kuacha ujumbe wa faraja.

Risiti ya asante

Unapokea ujumbe wa asante kwa WhatsApp au SMS wenye kumbukumbu ya muamala wako.

Habari za maendeleo

Kampeni uliyochangia ikifikia 25%, 50%, 75% au lengo lake, unajulishwa ili ushare tena.

Ripoti kampeni yenye shaka

Kitufe cha "Ripoti kampeni hii" kwenye kila kampeni. Tunasimamisha malipo na kuchunguza.

Kwa wenye kampeni

Kila unachohitaji kuchangisha, kushare na kupokea fedha.

Anzisha kwa dakika chache

Hadithi, picha halisi, lengo na tarehe ya mwisho. Unaweza kuchangisha kwa ajili yako au kwa niaba ya mtu mwingine.

Share kila mahali

WhatsApp, Facebook, X, Telegram, SMS au nakili link. Kila link inaonyesha picha ya kampeni na maendeleo yake ikishirikiwa.

Picha za hatua zenye QR

Kampeni ikifikia 25%, 50%, 75% na 100% unapata picha ya mraba tayari kwa WhatsApp Status na Instagram, yenye QR code ya kuchangia.

Dashibodi ya michango

Michango kwa wakati halisi, makato ya kila muamala, kiasi unachopokea na salio linalopatikana.

Taarifa kila mchango

Unajulishwa kila mchango unapoingia na kila hatua inayofikiwa.

Pokea fedha

Mobile money au benki, kwenye akaunti iliyokaguliwa. Ada ya kutoa TZS 1,500, kiwango cha chini TZS 10,000.

Kwa NGO na taasisi

NGO, CBO, taasisi za dini, foundation na shule.

Ukurasa wenu wenyewe

Link mnayoichagua (changisha.co.tz/o/jina-lenu), logo, picha ya bango, historia na mawasiliano. Mkibadilisha link, ya zamani inaendelea kufanya kazi.

Mfuko endelevu

Kitufe cha "Changia" kisicho na tarehe ya mwisho kwa kazi za kila siku za taasisi.

Kampeni nyingi za miradi

Anzisheni kampeni kadiri mnavyotaka chini ya jina la taasisi — bila barua ya Serikali ya Mtaa.

Alama ya uthibitisho

Baada ya kukagua usajili, TIN na barua ya viongozi, taasisi na kampeni zake zinapata alama ya bluu ya uthibitisho.

Orodha ya taasisi

Taasisi zilizothibitishwa zinaonekana kwenye orodha ya umma ambapo wafadhili wanaweza kutafuta kwa aina na mkoa.

Uaminifu na usalama

Tunakagua kabla fedha hazijatoka — si baadaye.

Uthibitisho wa utambulisho

Simu kwa SMS, NIDA, picha ya kitambulisho na selfie ukiwa umekishika.

Nyaraka na picha halisi

Barua ya hospitali au shule, makadirio ya gharama, picha ya hali halisi na barua ya Serikali ya Mtaa — zote hukaguliwa na admin.

Malipo yanayodhibitiwa

Fedha hulipwa kwenye akaunti iliyokaguliwa pekee, kwa awamu hadi TZS 1,000,000, na awamu inayofuata inahitaji risiti za matumizi.

Uwazi hadharani

Kila kampeni inaonyesha kiasi kilichochangwa na kiasi kilichokwisha tolewa kwa mlengwa.

Ulinzi wa taarifa

Nyaraka za utambulisho huhifadhiwa kwa siri kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2022). Wasimamizi wanaingia kwa uthibitisho wa hatua mbili.

Malipo na ada

Ada chache, zilizo wazi.

Ada ya huduma

5% ya jukwaa pamoja na gharama ya mtandao wa malipo — inalipwa na mchangiaji juu ya mchango, hivyo kampeni inapokea yote.

Bahshishi ya hiari

Mchangiaji anaweza kuongeza bahshishi kusaidia jukwaa — si lazima.

Kufungua ni bure

Hakuna ada ya kufungua akaunti, kuanzisha kampeni wala kusajili taasisi.

Ripoti na kumbukumbu

Kila shilingi inaweza kufuatiliwa.

Ripoti za PDF zenye nembo

Ripoti za michango zenye muhtasari, kumbukumbu za kila muamala na namba za kurasa — tayari kwa bodi, wafadhili au ukaguzi.

Excel (CSV)

Pakua data yote ya michango kwa uchambuzi wako mwenyewe.

Kumbukumbu za muamala

Kila mchango una namba ya kumbukumbu inayoweza kuhakikiwa kwenye mtandao wa malipo.

Rahisi kutumia

Imetengenezwa kwa simu kwanza.

Kiswahili na English

Badilisha lugha wakati wowote kwa kitufe cha SW/EN.

Mwanga, giza au kama simu

Chagua mwonekano unaokufaa kwenye menyu ya akaunti yako.

Ingia na Google

Jisajili kwa kubofya mara moja na picha yako ya Google inatumika kwenye akaunti.

WhatsApp na SMS

Taarifa muhimu zinakufikia kwa WhatsApp; zisipofika, kwa SMS.

Tayari kuanza?

Anzisha kampeni yako au sajili taasisi yako leo — ni bure.

Anzisha kampeni Sajili taasisi