Kuchangisha fedha za matibabu
Bili ya hospitali, upasuaji, dawa au matibabu nje ya mkoa — anzisha kampeni ya matibabu na uwaruhusu ndugu, marafiki na hata watu wasiokujua kuchangia kwa mobile money.
Nyaraka zinazohitajika
- Hospital letter / doctor’s report
- Cost estimate / invoice
- Photo of the real situation (beneficiary / event)
- Letter from the local government / ward executive
Pamoja na nyaraka hizi, mmiliki wa kampeni anathibitisha utambulisho wake kwa NIDA, picha ya kitambulisho na selfie. Ukichangisha kwa ajili ya mgonjwa mwingine, utahitaji pia ridhaa yake.
Jinsi ya kuandika kampeni ya matibabu inayoaminika
- Eleza ugonjwa au tatizo kwa lugha rahisi, hospitali anayotibiwa na daktari aliyependekeza matibabu.
- Onyesha mchanganuo wa gharama: upasuaji, dawa, kulazwa, usafiri — na weka lengo linalolingana na invoice.
- Weka picha halisi ya mgonjwa au hali yake (kwa ridhaa yake), si picha ya mtandaoni.
- Toa taarifa za maendeleo baada ya upasuaji au matibabu; wachangiaji wanapenda kujua walichosaidia.
Fedha zinaweza kwenda moja kwa moja hospitali?
Ndiyo. Akaunti ya kupokea fedha inaweza kuwa ya mgonjwa au ya hospitali husika, na inathibitishwa wakati wa kukagua kampeni. Benki inapokea kiasi chote kwa mara moja; mobile money inapokea hadi TZS 5,000,000 kwa siku.
Kampeni zinazoendelea
Jenga CHANGISHA APP — tusaidie kuendesha jukwaa la kuchangia la Kitanzania
CHANGISHA APP ni jukwaa la Kitanzania linalomwezesha mtu yeyote mwenye uhitaji halisi — matibabu, ada za shul…
WEZESHA ADA YA SHULE
Ndugu jamaa, marafiki na wadau, Natumaini mko salama. Naomba msaada wenu wa kifedha ili kufanikisha malipo…
Maswali ya mara kwa mara
Kampeni ya matibabu inaidhinishwa kwa muda gani?
Mara tu nyaraka zote zikiwa zimepakiwa na utambulisho wako umethibitishwa, timu yetu inakagua — mara nyingi tunapiga simu hospitali kuthibitisha. Kamilisha nyaraka mapema ili kampeni ianze haraka.
Je, mchangiaji anahitaji akaunti?
Hapana. Anachagua kiasi, anaweka namba ya simu na kuthibitisha kwa PIN ya M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa.
Ada ni kiasi gani?
Kuanzisha kampeni ni bure. Mchangiaji analipa ada ya huduma juu ya mchango (5% + takriban 2.57% ya mtandao), hivyo mgonjwa anapokea mchango wote.
Uko tayari kuanza?
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Maswali? Tupigie 0678515121