Michango ya msiba mtandaoni
Wakati wa msiba familia haina muda wa kufuatilia meseji za M-Pesa moja moja. Kwa CHANGISHA kila mchango unarekodiwa na kuonekana, kila mchangiaji anashukuriwa kiotomatiki, na kamati inaona jumla papo hapo.
Nyaraka zinazohitajika
- Picha ya hali halisi (mlengwa / tukio)
- Barua ya Serikali ya Mtaa / Mtendaji wa Kata
Kwa sababu ya uharaka wa msiba, andaa nyaraka mapema: barua ya Serikali ya Mtaa, picha, na utambulisho wa anayesimamia kampeni. Kibali cha mazishi au cheti cha kifo kinasaidia ukaguzi kuwa wa haraka zaidi.
Faida kwa kamati ya msiba
- Orodha ya wachangiaji na kiasi chao — pakua Excel au PDF wakati wowote kwa ajili ya taarifa ya kamati.
- Ndugu walio mbali wanachangia kwa simu bila kusafiri wala kutuma kwa mtu wa kati.
- Kila mchangiaji anapokea risiti ya asante kwa WhatsApp au SMS.
- Uwazi: kila mtu anaona kiasi kilichochangwa, hivyo hakuna maswali baadaye.
Kampeni zinazoendelea
Jenga CHANGISHA APP — tusaidie kuendesha jukwaa la kuchangia la Kitanzania
CHANGISHA APP ni jukwaa la Kitanzania linalomwezesha mtu yeyote mwenye uhitaji halisi — matibabu, ada za shul…
WEZESHA ADA YA SHULE
Ndugu jamaa, marafiki na wadau, Natumaini mko salama. Naomba msaada wenu wa kifedha ili kufanikisha malipo…
Maswali ya mara kwa mara
Kampeni ya msiba inaweza kuanza haraka?
Kila kampeni inakaguliwa kabla ya kupokea michango ili kulinda wachangiaji. Ukipakia nyaraka zote mara moja na utambulisho wako ukiwa umethibitishwa, ukaguzi unakuwa wa haraka.
Ni nani anapokea fedha?
Fedha zinalipwa kwenye akaunti iliyothibitishwa ya msimamizi wa msiba au ya familia, baada ya kila ombi kukaguliwa.
Wachangiaji wanalipa ada?
Ndiyo, ada ndogo ya huduma juu ya mchango (5% + takriban 2.57% ya mtandao), hivyo familia inapokea mchango wote.
Uko tayari kuanza?
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Maswali? Tupigie 0678515121