Kuchangisha fedha za dharura
Nyumba imeungua, mafuriko yamesomba mali, au ajali imetokea — kampeni ya dharura inakusaidia kukusanya msaada haraka kutoka kwa jamii na watu wenye moyo wa kusaidia.
Nyaraka zinazohitajika
- Picha ya hali halisi (mlengwa / tukio)
- Barua ya Serikali ya Mtaa / Mtendaji wa Kata
Vidokezo
- Eleza kilichotokea, lini na wapi, na mahitaji ya haraka (malazi, chakula, matibabu, vifaa).
- Weka picha halisi za tukio — zinajenga imani kuliko maneno.
- Weka lengo linaloeleweka na toa taarifa jinsi msaada ulivyotumika.
- Kwa majanga yanayogusa jamii nzima, taasisi iliyosajiliwa inaweza kuendesha kampeni kwa niaba ya waathirika.
Kampeni zinazoendelea
Jenga CHANGISHA APP — tusaidie kuendesha jukwaa la kuchangia la Kitanzania
CHANGISHA APP ni jukwaa la Kitanzania linalomwezesha mtu yeyote mwenye uhitaji halisi — matibabu, ada za shul…
Changia
WEZESHA ADA YA SHULE
Ndugu jamaa, marafiki na wadau, Natumaini mko salama. Naomba msaada wenu wa kifedha ili kufanikisha malipo…
Changia
Maswali ya mara kwa mara
Ni nyaraka gani zinakubalika kwa dharura?
RB ya polisi au barua ya Serikali ya Mtaa / Mtendaji wa Kata inayothibitisha tukio, pamoja na picha ya hali halisi.
Fedha zinapokelewa vipi?
Kwenye akaunti iliyothibitishwa ya mlengwa: benki kiasi chote kwa mara moja, au mobile money hadi TZS 5,000,000 kwa siku.
Uko tayari kuanza?
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Maswali? Tupigie 0678515121