Jinsi ya kuchangisha fedha mtandaoni kwa M-Pesa
Kwa CHANGISHA unachangisha fedha za matibabu, ada, msiba, dharura au mradi wa jamii. Watu wanachangia kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa, na kila mchango unaonekana papo hapo.
Hatua 5 za kuanza
- Fungua akaunti
Jisajili kwa email au Google, kisha thibitisha namba yako ya simu kwa code inayokuja kwa SMS au WhatsApp.
- Anzisha kampeni
Andika kichwa kinachoeleweka, eleza hali halisi na fedha zitatumikaje, weka lengo (angalau TZS 100,000) na picha kuu.
- Thibitisha utambulisho na pakia nyaraka
NIDA, picha ya kitambulisho na selfie, pamoja na nyaraka za kampeni kama barua ya hospitali au fee structure. Timu yetu inakagua kabla kampeni haijaanza kupokea michango.
- Share link na QR code
Tuma link kwenye makundi ya WhatsApp, Status, Facebook, Instagram na TikTok, au chapisha bango lenye QR code kwa ajili ya mikutano na ibada.
- Pokea na toa fedha
Kila mchango unathibitishwa papo hapo. Omba malipo kwenda mobile money au benki; kila ombi hukaguliwa kabla fedha hazijatumwa.
Mchangiaji analipaje?
Mchangiaji hahitaji akaunti wala app. Anafungua link ya kampeni, anachagua kiasi, anaandika jina na namba ya simu, kisha anathibitisha kwa PIN ya mobile money yake. Anapokea risiti ya asante kwa WhatsApp au SMS yenye kumbukumbu ya muamala. Anaweza pia kuchangia bila jina lake kuonekana.
- M-Pesa (Vodacom)
- Mixx by Yas
- Airtel Money
- HaloPesa
Kwa nini isiwe namba ya simu tu?
- Hakuna kufuatilia meseji za M-Pesa moja moja: kila mchango unarekodiwa na kuonekana kwenye ukurasa wa kampeni.
- Wachangiaji wanaona kiasi kilichochangwa na kilichotolewa, hivyo wanaamini na kuchangia tena.
- Kila mchangiaji anashukuriwa kiotomatiki, na wewe unajulishwa kila mchango unapoingia.
- Kampeni zinathibitishwa, hivyo hata watu wasiokujua wanaweza kuchangia kwa kujiamini.
Ada
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Mchangiaji analipa ada ya huduma juu ya mchango wake (5% ya jukwaa, angalau TZS 100, na takriban 2.57% ya mtandao wa malipo), hivyo kampeni inapokea mchango wote. Unapotoa fedha, mtoa huduma wa malipo anakata TZS 1,500 kwa kila ombi; kiwango cha chini cha kutoa ni TZS 50,000.
Miongozo kwa aina ya kampeni
Kampeni zinazoendelea
Jenga CHANGISHA APP — tusaidie kuendesha jukwaa la kuchangia la Kitanzania
CHANGISHA APP ni jukwaa la Kitanzania linalomwezesha mtu yeyote mwenye uhitaji halisi — matibabu, ada za shul…
WEZESHA ADA YA SHULE
Ndugu jamaa, marafiki na wadau, Natumaini mko salama. Naomba msaada wenu wa kifedha ili kufanikisha malipo…
Maswali ya mara kwa mara
Je, mchangiaji anahitaji kujisajili?
Hapana. Anaweka kiasi, jina na namba ya simu, kisha anathibitisha kwa PIN ya mobile money. Hakuna app wala akaunti.
Fedha zinafika lini kwangu?
Michango inaonekana papo hapo. Kampeni ikishathibitishwa unaomba malipo wakati wowote, na kila ombi hukaguliwa kabla ya kutumwa. Benki inapokea kiasi chote kwa mara moja; mobile money inapokea hadi TZS 5,000,000 kwa siku.
Ninaweza kuchangisha kwa ajili ya mtu mwingine?
Ndiyo. Utahitaji ridhaa ya mlengwa pamoja na nyaraka za hali yake, na fedha zinalipwa kwenye akaunti ya mlengwa au ya taasisi husika (mf. hospitali au shule).
Kampeni inachukua muda gani kuidhinishwa?
Inategemea ukamilifu wa nyaraka zako. Ukikamilisha mahitaji yote, timu yetu inakagua haraka. Ukikosa mahitaji kwa siku 30, kampeni inarudishwa kwako kama rasimu ili uikamilishe na kuiwasilisha tena.
Je, CHANGISHA ni salama?
Kila kampeni na kila taasisi inathibitishwa kabla ya kupokea michango, fedha zinalipwa kwenye akaunti iliyothibitishwa tu, na taarifa zako zinalindwa kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2022).
Uko tayari kuanza?
Kufungua akaunti na kampeni ni bure. Maswali? Tupigie 0678515121